1
Ufunuo 3:20
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu yeyote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami.
Linganisha
Chunguza Ufunuo 3:20
2
Ufunuo 3:15-16
Nayajua matendo yako, kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa moto au baridi. Hivyo kwa kuwa u vuguvugu, si baridi wala moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu.
Chunguza Ufunuo 3:15-16
3
Ufunuo 3:19
Wale ninaowapenda, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu.
Chunguza Ufunuo 3:19
4
Ufunuo 3:8
Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno langu wala hukulikana Jina langu.
Chunguza Ufunuo 3:8
5
Ufunuo 3:21
Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi.
Chunguza Ufunuo 3:21
6
Ufunuo 3:17
Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi.
Chunguza Ufunuo 3:17
7
Ufunuo 3:10
Kwa kuwa umeshika amri yangu ya kuvumilia katika saburi, nitakulinda katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote, ili kuwajaribu wote wanaoishi duniani.
Chunguza Ufunuo 3:10
8
Ufunuo 3:11
Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akalichukua taji lako.
Chunguza Ufunuo 3:11
9
Ufunuo 3:2
Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu.
Chunguza Ufunuo 3:2
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video