Lakini hesabu ya matofali, waliyoyafanya siku zote, sharti mwabandikie iyo hiyo, msiipunguguze! Kwani ndio walegevu, kwa hiyo hupiga kelele kwamba: Twende kumtambikia Mungu wetu! Kazi za utumwa sharti ziwalemee zaidi watu hawa, wakizifanya, wasitazamie maneno ya uwongo.