1
Mwanzo 26:3
Neno: Maandiko Matakatifu
Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
Linganisha
Chunguza Mwanzo 26:3
2
Mwanzo 26:4-5
Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, kwa sababu Ibrahimu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.”
Chunguza Mwanzo 26:4-5
3
Mwanzo 26:22
Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi, akisema, “Sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”
Chunguza Mwanzo 26:22
4
Mwanzo 26:2
BWANA akamtokea Isaka, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia.
Chunguza Mwanzo 26:2
5
Mwanzo 26:25
Isaka akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima.
Chunguza Mwanzo 26:25
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video