1
1 Wakorintho 15:58
Biblia Habari Njema
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Linganisha
Chunguza 1 Wakorintho 15:58
2
1 Wakorintho 15:57
Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Chunguza 1 Wakorintho 15:57
3
1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.
Chunguza 1 Wakorintho 15:33
4
1 Wakorintho 15:10
Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.
Chunguza 1 Wakorintho 15:10
5
1 Wakorintho 15:55-56
“Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?” Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria.
Chunguza 1 Wakorintho 15:55-56
6
1 Wakorintho 15:51-52
Sikilizeni, nawaambieni siri: Sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa, wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana tarumbeta ya mwisho itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa.
Chunguza 1 Wakorintho 15:51-52
7
1 Wakorintho 15:21-22
Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka kwa wafu kumesababishwa na mtu mmoja. Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo.
Chunguza 1 Wakorintho 15:21-22
8
1 Wakorintho 15:53
Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.
Chunguza 1 Wakorintho 15:53
9
1 Wakorintho 15:25-26
Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda maadui zake wote na kuwaweka chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.
Chunguza 1 Wakorintho 15:25-26
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video