Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 89:19-37

Zab 89:19-37 SUV

Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu. Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka. Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kuume juu ya mito. Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu litafanyika amini kwake. Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 89:19-37