Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 89:19-37

Zaburi 89:19-37 BHN

Zamani ulinena katika maono, ukawaambia watumishi wako waaminifu: “Nimempa nguvu shujaa mmoja, nimemkuza huyo niliyemteua kati ya watu. Nimempata Daudi, mtumishi wangu; nimemweka wakfu kwa mafuta yangu matakatifu. Mkono wangu wa nguvu utakuwa naye daima; mkono wangu mimi mwenyewe utamwimarisha. Maadui hawataweza kumshinda, wala waovu hawatamnyanyasa. Mimi nitawaponda wapinzani wake; nitawaangamiza wote wanaomchukia. Nitakuwa mwaminifu kwake na kumfadhili, kwa jina langu atapata ushindi mkubwa. Nitaimarisha nguvu na utawala wake, toka bahari hata mito. Yeye ataniita: ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu.’ Nami nitamfanya kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, mkuu kuliko wafalme wote duniani. Fadhili zangu nitamwekea milele, na agano langu kwake litadumu daima. Nitaudumisha daima ukoo wake wa kifalme, na ufalme wake kama mbingu. “Lakini wazawa wake wakiiacha sheria yangu, wasipoishi kadiri ya maagizo yangu, kama wakizivunja kanuni zangu, na kuacha kutii amri zangu, hapo nitawaadhibu makosa yao; nitawapiga kwa sababu ya uovu wao. Lakini sitaacha kumfadhili Daudi, wala kuwa mwongo kuhusu uaminifu wangu. Sitavunja agano langu naye, wala kubatili neno nililotamka kwa mdomo wangu. “Nimeapa mara moja tu kwa utakatifu wangu; nami sitamwambia Daudi uongo. Ukoo wake utadumu milele; na ufalme wake kama jua. Utadumu milele kama mwezi utokezavyo angani.”

Soma Zaburi 89

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 89:19-37