Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 89:19-37

Zaburi 89:19-37 SRUV

Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu. Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka. Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kulia juu ya mito. Yeye ataniita, Wewe ni baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wote wa dunia. Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu naye litadumu hata milele. Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizivunja amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. Mimi sitalivunja agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, Wazawa wake watadumu milele, Na kiti chake cha enzi kuwa mbele yangu kama jua. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni.

Soma Zaburi 89

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 89:19-37