Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Mambo yanapoonekana kuwa magumu, ndipo msaada wa Mungu huhitajika. Ndivyo alivyowaza mpagani Nebukadreza. Hiyo ilimpa Danieli nafasi ya kushuhudia juu ya maarifa ya Mungu aliye hai. Ndoto ya mfalme ilihitajiwa kutafsiriwa, lakini waganga wote walikwama kuitambua na kuitafsiri. Ikaamriwa wapotezwe uhai wao. Danieli anajitokeza kuokoa. Anaomba kibali apate kutafakari, baada ya wengine kushindwa. Kwa nini? Kwa sababu miungu yao haiishi na watu. Rudia m.11, na tafakari tofauti yake na 5:11: Yuko mtu katika ufalme wako, [Ee mfalme], ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/