Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa (m.26). “Kwetu sisi”ni nani? Wana wa ukoo wa Ibrahimuni Wayahudi. Wanaomcha Munguni mtu wa taifa lolote ambaye anamwamini Mungu wa Wayahudi, kama yule Kornelio (10:1-2). Kwa hiyo “kwetu sisi”ni watu wa mataifa yote. Kwa hao wote, hata Watanzania, wokovu huu umeletwa: Msamaha wa dhambi; na kwa [Yesu]kila amwaminiye huhesabiwa haki (m.38-39) Je, umeupokea?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/