Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia (m.2). Ufunuo huu bila shaka ulitolewa na mmoja wa manabii wao. Wakati Sauli alipookoka, Yesu alimjulisha wajibu wake kwamba atafanya kazi ya misioni (Mdo 9:15). Miaka iliyofuata Mungu alikuwa anamwandaa kwa kazi hii. Sasa muda wake ulikuwa umefika, na kanisa lilithibitisha wito wake na kumtuma. Mtu binafsi kupewa wito pamoja na uongozi wa kanisa kutoa wito ni vitu viwili vinavyokwenda pamoja kwa uongozi wa Roho (m.4)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/