Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Sauli alikuwa mwenyeji wa Tarso. Alikuwa ni Myahudi safi (kama alivyojitambulisha mwenyewe, Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia; Flp 3:5-6), lakini pia ni raia wa dola ya Rumi. Kwa hiyo zaidi ya Sauli(Kiebrania) pia alikuwa na jina la Kilatini: Paulo(m.9). Kilatini ni lugha ya Warumi. Katika Matendo ya Mitume twasoma juu ya safari nne za Paulo. Safari tatu zilikuwa za misioni. Kila sehemu aliposafiri ni chini ya dola ya Rumi! Kwenye kila safari alikuwa anafika jimbo la Asiaambalo siku hizi liko chini ya nchi ya Uturuki. Kama ukiwa na Biblia, tazama ramani ya safari za Paulo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/