Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Mfalme Dario alimhakikishia Danieli kuwa Mungu amtumainiye atamwokoa. Hata alifunga kwa ajili yake; ila Dario hakupata amani mpaka alipoenda kwenye tundu lile na kushuhudia kuwa Danieli yu salama. Hebu, zingatia ushuhuda huu: Mungu wangu amemtuma malaika wake naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru, kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno(m.22). Wokovu wa Danieli ukawa ushuhuda kwa mataifa yote (m.25-27).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/