Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Asafu anaendelea kueleza alivyotaabika kuhusu mafanikio ya waovu. Alitaka kumwacha Mungu, akiona hakuna faida ya kumtumikia (m.13-16). Mwishowe Asafu alipata jibu kuwa mwisho wa maisha ya waovu ni maangamizo (m.18-19). Je, umewahi kujaribiwa ukiona mafanikio ya waovu? Zaburi hii inatufundisha kuwa kama wewe umeokoka usitahayari. Kutahayari ni upumbavu (m.21-23). Kumbuka pia kuwa, katika Kristo, Mungu ametujalia zawadi zote za kiroho (Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; Efe 1:3). Mshukuru Mungu kwa baraka hizo badala ya kutamani mambo ya dunia (m.23-24).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/