Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 24 YA 31

Danieli anamheshimu Mungu kwa kuzikataa zawadi zile ambazo Belshaza amemwahidi yule awezaye kumtafsiria ndoto yake (m.17). Mfalme anaelezwa kuwa hali mbaya iliyopo ni mwendelezo wa uovu wa babaye Nebukadreza. Alipofanikiwa aliota kiburi, lakini baadaye alijinyenyekeza Mungu alipomwadhibu. Unyenyekevu huo mwanawe ameukosa (m.23). Kwa vile Belshaza ametumia visivyo vyombo vya Bwana, matokeo yake ni kuuawa. Nafasi yake ikachukuliwa na Dario. Ujumbe huu unawahusu wote wamkataao Mungu.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/