Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha(m.5). Hayo ni mafundisho ya maana kwa Wakristo wote. Yesu anasema:"Mtu akinitumikia, na anifuate" (Yn 12:26). Kuufuata wito wa Bwana ni kujiweka chini ya mapenzi yake ili jina la Bwana litukuzwe kwa maisha yetu. Wito unaweza kutuletea taabu na hatari pia, kwa sababu tunapigana vita na shetani, lakini tunajua daima kwamba mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Yeye ni mshindaji mkuu, na tunamtegemea atoe maji katika eneo la ukame (m.4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/