Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Kunahitajika ujasiri na hekima ya ziada kuthubutu kuingia na kusimama mbele ya matawala kama Nebukadreza na kumpa ujumbe usio wa matumaini bali maangamizi (soma m.25). Mungu ndiye mmiliki wa uumbaji wote, na si mwanadamu. Mungu anagawa mamlaka kwa anayemtaka yeye. Wale anaowaruhusu watawale ni wale wanaojua na kukubali kuwa mwenye mamlaka yuko juu yao. Sharti la mfalme kuendelea kubaki kitini ni kutubu dhambi, kutenda haki na kuhurumia maskini. Nje ya hayo hakuna kudumu. Rudia m.27.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/