Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 6 YA 30

Musa alitunga wimbo uliofafanua kwanza jinsi Mungu alivyojitoa kwa ajili ya taifa la Israeli kwa kila njia. Leo uyazingatie maneno yanayotumika kueleza upendo mkuu wa Bwana. Alimkuta, alimzunguka na kumtunza na kumhifadhi kama mboni ya jicho(m.10). Tena akamtwaaIsraeli kama tai anavyoyachukua makinda yake (m.11:Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; na kupapatika juu ya makinda yake, [Bwana]alikunjua mbawa zake, akawatwaa [Waisraeli], akawachukua juu ya mbawa zake). Alimwongoza hadi mahali pema sana na kuendelea kumnyonyeshakila aina ya chakula (m.12-14: Bwana peke yake alimwongoza [Waisraeli], wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye. Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, naye akala mazao ya mashamba; akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume; siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo, pamoja na mafuta ya wana-kondoo, kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi, na unono wa ngano iliyo nzuri; ukanywa divai, damu ya mizabibu). Ni maneno yanayothibitisha upendo wake. Hivyo uasi na uakaidi wa Israeli ni wa ajabu kabisa. 

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

Mipango inayo husiana