Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 8 YA 30

Yule “kahaba” katika m.26b ni mke wa mtu mwingine. Hivyo mstari huo unasema kuwa kuzini na malaya ni dhambi mbaya; hata hivyo matokeo ya kumkumbatia mke aliyeolewa ni mabaya zaidi. Ni kama mkaa kifuani petu. Hakika tunajiunguza. Anayezini na mwanandoa, kwanza anajiangamiza mwenyewe:Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake(m.32). Pia kuna madhara ya kumwumiza mwenzi wa mwanandoa tunayeshirikiana naye kikahaba. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi(m.34). Na ikiwa tumefunga ndoa sisi wenyewe, hata ndoa yetu iko hatarini. Si vigumu kuona madhara haya. Tuonyeke.

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz

Mipango inayo husiana