SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Watu wengi wanazungumza kuhusu maneno yaliyo katika sura ya 5 hadi 7 kama Hotuba ya mlimaniya Yesu. Kuna mistari tisa inayoanza na neno heri, ambalo ni sawa na kusema "amebarikiwa”. Kuwa maskini wa roho, mwenye huzuni, mpole, na mwenye njaa ya kiu ya haki, ni sifa ya mtu aliyepondeka moyo na kujitambua kuwa akiwa peke yake hawezi kukabiliana na mambo yanayomkabili katika maisha. Anachohitaji ni kupokea uweza wa Bwana unaomsaidia kusonga mbele katika safari. Utoshelevu wa Mkristo upo katika hali ya kujua kwamba anamhitaji Yesu kwa kila jambo na Yesu hatamwacha awe peke yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz