SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Nyota iliwaongoza mamajusi kwenda Yerusalemu kuuliza, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi?(m.2). Lakini angalia kuwa ni nuru ya Neno la Munguiliyowafikisha Bethlehemu ambako walimkuta mtoto! Hapo wakamsujudia, wakamtolea zawadi. Hii ni mara ya kwanza Yesu kujifunua kwa mataifa kwamba yeye ni mwokozi wa ulimwengu. Kila anayefuata nuru kama hao mamajusi, hatakosa kumwona Yesu, kumwabudu na kumtukuza. Je, wewe unamtafuta ili kufanya hivyo? Umeandaa zawadi gani kwake? Miili na roho zetu ndiyo dhabihu iliyo hai inayompendeza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz