Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

SIKU 2 YA 31

Kitabu hiki cha ukoo wa Yesu kiliandikwa ili kuthibitisha kuwa Yesu ni mwanadamu kweli. Kwa Wayahudi wengi alikuwa mtu wa kawaida tu, na Pilato alimlinganisha hata na Baraba. Lakini ukoo huo, ulipata baraka za Mungu zilizoyafikia mataifa yote; maana kutokana na ukoo huo, mkombozi wa dunia nzima alizaliwa. Mungu ametushirikisha baraka zake sawa sawa na unabii wa Isa 7:14,Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.Ndivyo malaika anavyokumbusha Yusufu katika Mt 1:23. Yesu ni "Imanueli", maana yake, ni "Mungu pamoja na wanadamu". Tofauti yake na sisi ni jinsi alivyochukuliwa mimba tu: Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu(m.18).

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz