Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

SIKU 4 YA 31

Yesu alizaliwa kuwa Mfalme wa Wayahudi, wakati Mfalme Herode alipotawala. Soma pia Yn 18:36-37 kuelewa ufalme wa Yesu ulivyo. “Mamajusi” maana yake ni “wenye hekima”. Walifika Yerusalemu wakiongozwa na nyota. Walimwuliza Mfalme Herode, Yuko wapi Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa? Herode alifadhaika sana na maelezo yao. Alifikiri atanyang’anywa ufalme, akaanza kuhangaika akiita watu maarufu ili kuwauliza, Kristo azaliwa wapi?"Kristo", maana yake ni "mpakwa mafuta wa Bwana". Yaani Yesu ni Mfalme aliyepewa kutimiza unabii wa Isaya 9:6-7 unaosema, Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz