SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Kwa kuwa Mungu alifahamu nia mbaya ya Mfalme Herode, alimtokea Yusufu kumwambia amchukue mtoto na wakimbilie Misri ili Herode asimwangamize Yesu katika hila yake. Yesu alizaliwa kwa kusudi maalumu la Mungu ili aokoe ulimwengu na dhambi. Yusufu alitii, akakaa Misri mpaka Herode alipokufa, sawa na unabii wa Hos 11:1 ambapo Mungu anasema, Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri. Hasira za Herode kwa kutokuweza kumwua mtoto Yesu, zilimfanya awaue watoto wote wa kiume wa miaka miwili kwenda chini huko Bethlehemu. Alisababisha maafa makubwa yaliyosababisha maombolezo makuu, sawa na unabii katika Yer 31:15 ambapo Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz