SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Hali yetu ya kibinadamu inatufanya kuyaona zaidi makosa au udhaifu wa wengine. Hata tunakuwa wepesi wa kulaumu na kuwahukumu wengine. Neno la Mungu linatuonya kwamba anayeweza kuona na kutoa hukumu ya kweli ni Mungu mwenyewe, siyo mwanadamu. Na hapo ni lazima tujue kuwa maovu ya kila mtu yapo wazi mbele za Mungu. Na pia tufahamu kuwa Yesu anajua kuwa kuna wale wanaoliheshimu Neno la Mungu katika hali ya ukweli na ambao wanalidharau na kulitumia kwa malengo yao wenyewe. Basi, msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua(m.6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz