Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

SIKU 25 YA 31

Amri ya sita inasema, “Usizini”. Yesu anatoa mkazo juu ya amri hii kwamba isitazamwe katika hali ya nje tu, maana uovu huanzia ndani ya moyo wa mtu. Wakati wa Musa kulikuwa na tatizo la maisha ya ndoa. Hali hiyo ikapelekea kuruhusu mume kumpa talaka mke wake. Biblia inasema Musa alifanya hivi kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Huo haukuwa mpango wa Mungu. Tukisoma Mk 10:6-12 tunapata mafundisho ya ndoa ya Kikristo kwa mpango wa Mungu: Tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.  Kwa hiyo, wanandoa na watakaoingia katika ndoa baadaye wanapaswa kuishi kulingana na Neno la Mungu.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz