Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

SIKU 29 YA 31

Inatakiwa kuifanya kazi ya Mungu bila kuwa na unafiki wowote. Na hapo Yesu anataka tupate nafasi ya kujua kwamba, tunapofunga na kuomba, silo jambo la kujionyesha kwa wengine kwamba sisi ni wacha Mungu. Kuwa Mkristo wa kweli ni ile hali ya mtu kujitambua kwamba yeye mwenyewe hawezi lolote, ila anamhitaji Mungu aliye Mtakatifu. Tukisoma Yn 4:19-24, tunaelezwa namna tunavyotakiwa kuwa na nia na mawazo yanayotuelekeza kwa Mungu anayetuwazia yaliyo mema: Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz