SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20Mfano
Ujumbe maalumu wa Yohana Mbatizaji ulikuwa ni utii kwa unabii wa Isaya usemao: Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana. Ndivyo Yohana anavyojitambulisha katika Yn 1:23 akisema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. Yohana aliwaandaa watu kumpokea mkombozi wao ambaye ni Yesu. Wote walioungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani, akawaonya wazae matunda yapasayo toba. Wasijivune kuwa wakiwa tu wana wa Ibrahimu, baba wa imani, basi wamezaliwa kuwa watu wa Mungu. Maana Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto(m.9). Yaani, Mungu anaweza kutufanya sisi wa Mataifa kuwa wana wake; ila tusipozaa matunda ya toba vilevile sisi hatutaepuka hukumu yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 01/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Kutoka, Zaburi na Isaya. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Anza mwaka wa 2020 kwa kujifunza Neno la Mungu kupitia mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz