Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 15 YA 31

Huenda Nathani alikuwa nabii mshauri kwa mfalme Daudi. Wajibu wake unalingana na ule aliokuwa nao Samweli kwa mfalme Sauli. Tunasoma mara kwa mara kwamba Daudi alikuwa anamwuliza Bwana juu ya mipango yake (k.m. 5:19). Labda maana yake ni kwamba alimwuliza Nathani ambaye alikuwa anapata jibu kwa Bwana kama ilivyo katika somo la leo. Tunamkuta Daudi akiwa anastarehe katika nyumba yake nzuri. Ndipo akawaza kuwa huenda sasa muda ulikuwa umefika wa kumjengea Bwana nyumba nzuri? Lakini Bwana alikataa, akisema, Mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo(m.6).

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz