Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 16 YA 31

Mungu alikuwa na sababu mbili za kukataa wazo la Daudi. 1. Alikuwa bado hajamaliza kumjengeaDaudi nyumba, yaani kuuimarisha ufalme wake (m.11, BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba). Baadaye tutaona kuwa Daudi alikusanya mali nyingi iliyomwezesha mwana wake kulijenga hekalu. 2. Daudi alikuwa mfalme wa vita, alikuwa amemwaga damu nyingi (1 Nya 22:7-10, Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, … Neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu). Ila Bwana alimpa pia ahadi nzuri kuhusu ufalme wake na ukoo wake! Ilitimizwa kwanza kwa Sulemani aliyejenga hekalu. Lakini zaidi sana ilitimizwa kwa njia ya Yesu Kristo, kama malaika alivyomwambia Mariamu, Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho(Lk 1:32-33). Hivyo Yesu amekuwa pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi, mtumishi wakeMungu (Lk 1:69).

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz