Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 1 YA 31

Kitabu hiki chote kinamhusu Daudi akiwa mfalme. Tukio la kwanza ni Daudi kupata habari kwamba Sauli na jeshi lote la Israeli wamepigwa vibaya sana na Wafilisti. Aliyesimulia mambo hayo alichanganya uongo na ukweli (ling. 1 Sam 31:1-6 inayoeleza ifuatavyo: Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima wa Gilboa. Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye. Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo). Huyo aliyemsimulia Daudi alitegemea atafurahi na kumpongeza. Ikawa sivyo. Ndipo Daudi na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli (m.11-12). Daudi alimlilia adui yake mkuu, Sauli! Katika hili ni mfano wa Kristo aliyesema, Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka (Lk 13:34; ukitaka kutafakari zaidi jambo hili tafuta kusoma Soma Mt 5:43-44 na Lk 19:41-44).

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz