Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 6 YA 31

Fanya agano nami, na tazama, mkono wangu utakuwa pamoja nawe, ili kuwaleta Israeli wote kwako (m.12). Maneno haya ya Abneri kwa Daudi yanaonyesha kwamba aliyekuwa na mamlaka juu ya Israeli; ni yeye wala si Ishboshethi (m.11: Mfalme hakuweza kumjibu Abneri tena, kwa sababu alimwogopa). Na Abneri alifanikiwa kutekeleza ahadi yake; hata Wabenyamini, kabila la Sauli, walikubali kwenda upande wa Daudi (m.19, Abneri alinena masikioni mwa Benyamini ... maneno yote yaliyoonekana kuwa mema ... machoni pa nyumba yote ya Benyamini)! Abneri alikwisha tambua kuwa Daudi ana nguvu kuliko yeye, na alijua ni kwa sababu Bwana yu pamoja naye (m.9-10, 17 na 18 ambapo Abneri anasema,Bwana amemtaja Daudi, akisema, kwa mkono wa mtumishi wangu, Daudi, nitawaokoa watu wangu Israeli katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya adui zao wote). Kuhusu Mikali, unaweza kusoma katika 1 Samweli 18:27-29 na 25:44 ni kwa sababu gani Daudi anamwambia Abneri amletee (m.13-16).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz