Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Sisi tukisengenywa vibaya, hujaribiwa kutumia maneno makali yasiyo na hekima kwa kujibu masengenyo hayo. Ni tofauti na Daudi. Anaomba alindwe na dhambi hiyo. Hataki kufuata njia mbaya ya watu waovu. Iwapo mtu wa Mungu ana sababu ya kumkemea, Daudi anaomba wakati wowote apokee maneno hayo kuwa baraka kwake, kana kwamba amepakwa mafuta (m.5, Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani). Na mwenyewe, siku zote atapinga uovu. Huwa unatumia maneno gani kujibu, wakati unapokosolewa au kupingwa na walio kinyume nawe? Omba ufanane na Daudi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz