Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Daudi akawazaa wana huko Hebroni (m.2). Orodha katika m.2-5 inaonyesha kuwa hao wana sita aliwapata kwa wake sita tofauti. Huenda wana wake walikuwa wengi zaidi, maana wakati fulani walikuwa na desturi ya kumtaja tu mzaliwa wa kwanza kwa kila mke. Kwa Waisraeli ilikuwa dalili ya kubarikiwa na Mungu, mtu alipokuwa na watoto wengi (Zab 127:3-5, Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani. Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni). Wakati wa Agano la Kale Mungu aliruhusu mwanamume kuwa na wake wengi. Lakini Mwana wa Mungu amekataa jambo hili katika Mt 19:3-9, Basi Mafarisayo wakamwendea [Yesu], wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz