Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 3 YA 31

Daudi hakupata kuwa mfalme juu ya Israeli yote kwa mara moja. Akawa kwanza mfalme juu ya kabila lake tu (Wayuda). Kuna sababu mbili. 1. Abneri, kamanda wa jeshi la Sauli, alikuwa shujaa na mwenye mamlaka sana (kwa mfano imeandikwa katika m.9 kwamba Abneri akamweka [mwana wa Sauli] awe mfalme). Tena ni ndugu yake Sauli kiukoo. 2. Kawaida ni kwamba mtoto wa mfalme anaurithi ufalme mara mfalme akifa. Hivyo Ishboshethi akawa mfalme. Daudi alifanyaje? Daudi akauliza kwa Bwana (m.1), maana alikuwa amejiweka kabisa chini ya uongozi wa Bwana! Alimtegemea kwa kilajambo. Nasi tuige mfano wake!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz