Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 17 YA 31

Daudi aliguswa sana na ujumbe wa Bwana, akafanya kama mwenyewe ametuagiza katika Zab 62:8, Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu (Biblia ya Habari Njema).Daudi ni mnyenyekevu. Anajiona kuwa hastahili haya makubwa ambayo Bwana humfanyia (m.18: Daudi akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?). Daudi anatumia neno "mtumwa wako" hata mara kumi katika sala yake hii! Na anamtukuza sana Bwana (m.22-23; 26)! Na hiyo ndiyo shabaha kuu ya yote: jina la Bwana lisifiwe. Ameni!

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz