Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano
Ni bahati kwetu kwamba Yesu mwenyewe ameufafanua mfano huu katika m.36-43. Unashauriwa kuisoma mistari hii kabla ya kuendelea na maelezo haya! Mfano hausemi juu ya wana wa ufalme wa Mungu na wana wa yule mwovu kuishi pamoja ndani ya kanisa. Kuhusu jambo hili Yesu ametoa mafundisho katika Mt 18:15-17, akisema, Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Bali mfano huu unasema juu ya wana wa ufalme na wana wa yule mwovu kuishi pamoja katika ulimwengu huu. Angalia m.38 anaposema Yesu kwamba lile konde ni ulimwengu.Kwa mfano huu Yesu anakataza tabia ya kutaka kuendeleza ufalme wa Mungu katika ulimwengu huu kwa kutumia nguvu na mamlaka ya kidunia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz