Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 31 YA 31

Yesu anatufundisha tabia inayoleta heshima mbele ya Mungu. Ni tabia ya kuwajali sana wadogo hao waniaminio (m.6).Hao ni watoto. Tena ni mtu ye yote aliyekubali kujinyenyekeza na kumpokea Yesu kama Mwokozi wake. Yesu mwenyewe anaeleza hivi katika Mt 25:40 na 45,Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. ... Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Wengi wao si watu wenye vyeo. Kwa hiyo huitwa wadogo- au hata watoto wachangukama Yesu anavyowatambulisha katika Mt 11:25-26, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.Vilevile imeandikwa katika 1 Kor 1:26-31,Ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.Lakini Yesu yuko ndani yao, kwa hiyo ukiwapokea unampokea Yesu. Ukiwadharau unamdharau Yesu. Basi, tutafute kwanzakusifiwa kwa walio wa Yesu na si kwa wenye vyeo katika dunia hii!

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz