Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 24 YA 31

Mungu amesema hatasikiliza maombi ya wakaao Yerusalemu (8:18, Sitaona huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza). Hata hivyo inaonekana katika m.4 kwamba amewasikia wote wanaomlilia, wakiugua kwa sababu ya machukizo yaliyopo mjini, maana Bwana anamwambia malaika, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia. Waumini hao wanatiwa alama kabla malaika hawajatekeleza hukumu ya Mungu ili wasiuawe. Ndivyo Mungu alivyo katika neema yake. Ila hiyo isitufanye kuwaza kuwa Mungu haoni au hashughulikii vitu vidogovidogo kama masengenyo, uongo, matukano n.k. Ukweli ni kwamba Mungu aona yote, na hukumu yake itafanyika:Tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru(m.11).

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz