Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 25 YA 31

Kazi ya chachuinafanana na kazi ya hamira. Chachu kidogo tu ikiwekwa ndani ya unga uliokandwa itaenea katika unga wote na kuumua. Lakini chachu pia ni tofauti na hamira, maana chachu ina harufu ya uchungu ambayo inaibadilisha harufu yote ya unga wote. Mafundisho ya Mafarisayo ni kama chachu mbaya kwa wanafunzi, kwa hiyo wajilinde na mafundisho hayo! Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo(m.11-12). Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi hawakumtambua. Hii inaonyesha kwamba hawakuongozwa na Roho wa Mungu. Nasi tujilinde na chachu mbaya!

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz