Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano
Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (m.18). Hapa kuna faraja na kutiwa moyo kwa kila Mkristo anayepiga vita ya Bwana. Maana kanisa ni la nani? Ni la Petro? Ni la askofu? Ni la mchungaji? La! Kanisa ni la Yesu, kama anavyosema mwenyewe katika m.18,Kanisa langu. Na ni nani anayelijenga hilo kanisa? Ni Yesu. Angalia anavyokaza vilevile katika m.18, Nitalijenga kanisa langu. Kwa hiyo sisi ni wafanya kazi pamoja na Yesu. Anayejenga ni yeye, sisi ni vyombo vyake tu. Kwa hiyo twashinda! Zingatia jinsi jambo hili lilivyoelezwa katika 1 Kor 3:9,Sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. Na vilevile anayosema Yesu katika Yn 15:4-5,Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz