Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano
Watu wa Yerusalemu walisikia kuwa Bwana ameiacha nchi hii(m.12), na Mungu anathibitisha kwa Ezekieli kwamba ndivyo anavyoelekea kufanya (m.6: Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, hata niende zangu mbali na patakatifu pangu?). Tayari utukufu wa Mungu umeanza kuondoka jengo la hekalu (m.3-4: Roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu.Na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwapo hapo). Lakini wanaposema Mungu hawaoni, siyo kweli. Sababu ya kuwaacha ni yale maovu anayoona! Mifano minne inaonyesha hayo yameenea hata hekaluni mwa Mungu. Ndivyo hali ilivyo kwetu pia. Hata katika mahali pa ibada pamefanyika makao ya kumwabudu shetani na kupafanyia maasi. Tujisahihishe!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz