Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano
Fedha na mali ni zawadi atupazo Mungu ili kwa hizi tumtukuze. Lakini kama tukizitumia isivyokusudiwa, zitageuka kuwa kwazo la uovu(m.19), yaani, chanzo cha dhambi. Ipo mifano mingi: Elimu imetumika kupotosha watu. Miili imetumika kwa zinaa. Maarifa yametumika kudhulumu. Hata mahali pa siripametiwa unajisi (m.22). Neno la asili ni “hazina ya thamani kubwa” na kumaanisha hekalu la Mungu. Ona Mungu asemavyo katika 1 Fal 9:6-9 kuhusu hekalu lake, ukikumbuka kuwa muumini ni hekalu la Roho: Mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz