Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

SIKU 17 YA 30

Mungu ni mwenye rehema na yupo tayari kuwasamehe wale wote wanaotubu. Lakini bado anabaki na ghadhabu juu ya wale wasiotaka kutubu. Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana(m.38). Mungu halazimishi watu kumwabudu, ila anatoa fursa kwa kila anayetaka uzima wa milele kumsikiliza na kumfuata. Aidha anawaalika watu wote kumwabudu katika roho na kweli. Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote(m.40). Naye anaahidi kuwabariki wale walio tayari kumwabudu. Mpendwa msomaji, tamani kumwabudu Mungu, kuisikiliza sauti yake na kuyaishi maagizo yake. 

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz