Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Ezekieli anaelezea kuwa Mungu atakapoamua kuadhibu waliomwasi, hakuna atakayeweza kuiepuka ghadhabu hiyo (m.47-48, Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hata kaskazini zitateketezwa kwa moto huo. Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, Bwana, nimeuwasha; hautazimika). Ikumbukwe kuwa siku zote BWANA MUNGU anachukia uovu, na kila tutendapo uovu tunasababisha ghadhabu yake kuwaka juu yetu. Hata hivyo yeye ni mwingi wa rehema, anatualika kutubu.Ugua, basi, Ee mwanadamu; kwa kuvunjika kwake viuno vyako, na kwa uchungu, utaugua mbele ya macho yao(m.6). Hivyo msomaji wa somo hili leo, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Jitafakari juu ya mahusiano yako na Mungu, kisha tafuta kutubu na kuanza maisha mapya yapatanayo na toba.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz