Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Kuenea na kukua kwa Ukristo kumeambatana na mateso. Mateso haya yameleta au kusababisha vifo vya Wakristo wanaosimama imara kumshudia Kristo kwa wazi, kwa siri na kweli. (Ukiwa na nafasi, soma Mdo 6:8-15 na 7:54-60 kuhusu Stefano.) Mateso ya Wakristo yamekuwa chachu njema ya kueneza Injili ya Kristo. (Unaweza kusoma mfano katika Mdo 8:1-8.) Tunapokabiliana na matatizo katika maisha ya ufuasi, tusikate tamaa wala kurudi nyuma. Ushindi upo, kwa kuwa kazi ya Mungu haishindwi. Hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia(Isa 35:10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz