Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

SIKU 4 YA 30

Kama ilivyokuwa wakati wa kanisa la kwanza, leo pia tunakabiliana na wahubiri na waalimu wa uongo. Hawa wanajishughulisha zaidi na mambo yahusuyo heshima na utajiri wa ulimwengu huu. Paulo anasema hao hulighosi neno la Mungu (2 Kor 2:17, Sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo). Mkazo mkuu wa wahubiri na waalimu wa uongo ni kutaka kujinufaisha kwa njia ya mali, heshima na kujitwalia utukufu. Badala ya kujaa Roho Mtakatifu hujaa roho mtakavitu. Tunaweza kuwatambua hawa kwa njia ya kupima mafundisho na maisha yao. Neno la Mungu ndilo kipimo halisi. Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana (Yer 9:23-24; pia unaweza kusema Mt 7:15-22).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz