Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

SIKU 9 YA 30

Kazi ya Mungu hutendeka kwa urahisi ikiwa kuna maelewano ya kweli baina ya wahusika wakuu wa huduma hiyo. Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kuliwezesha Neno la Kristo kuichambua na kuipa changamoto (kuikosoa) mioyo yetu. Itikio la moyo uliokosolewa au kuonywa na Neno  la Mungu huwa ni toba. Kugeuka kutoka hali ya dhambi na kuishi maisha ya kuhitaji msamaha. Huzuni ya dhambi bila kutubu kwa kweli haisaidii katika hatua za kukua kiroho. Nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote.Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti(m.9-10).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz