Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Ugumu wa safari au jukumu lolote maishani isiwe sababu au kikwazo cha kuturudisha nyuma. Ufuasi wa Kikristo hasa katika kuitangaza Injili kunafuatana na vikwazo vya wazi na vya siri. Vikwazo vyaweza kutoka ndani yako binafsi, familia, kanisa, taifa, mwili, ulimwengu na Shetani. Watumishi wa Kristo Yesu husimama kidete hata wakati wa hatari. Tuwatie moyo na kuwaombea watumishi wa Neno la Kristo ili wasikate tamaa. Na sisi wenyewe tusiwakatishe tamaa. Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao(Ebr 13:7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz