Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Hapa tai mkubwa anasimama badala ya Mungu aliyepanda mbegu ya wokovu nayo ikawasaidia wengi (m.22-23, Bwana MUNGU asema hivi; Mimi nami nitakitwaa kilele kirefu cha mwerezi, na kukipandikiza mahali; na katika vitawi vyake vilivyo juu nitatwaa kitawi kimoja kilicho chororo, nami nitakipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana;juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi, na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi yake watakaa). Maana yake Mungu alimwinua ”Masihi” ambaye kwa njia yake ulimwengu wote ulipata wokovu na kubarikiwa. Mpendwa msomaji, tambua kuwa, kwa njia ya Yesu Kristo, Mungu anatupenda. Unapaswa kumshukuru na kuupokea wokovu huo kwa vitendo. Wanadamu hatuna sababu ya kuitegemea miungu wala watu wengine tena, maana kwa njia ya Kristo hao wote ni miti iliyoangushwa, haina nguvu tena (m.24, Miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, Bwana, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, Bwana, nimenena, nami nimelitenda jambo hili).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz