Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Nabii Ezekieli anawaasa Waisraeli kuwa maisha ya duniani ni ya kitambo kidogo na baada ya hapo kuna uzima mwingine ambao, wote wanaojitambua kuwa ni wenye dhambi wakatubu wataendelea kuishi vema hata katika ulimwengu ujao. Bali wanaojisahau na kuendeleza uovu watapotea milele. Kwa ujumbe huu Mungu anataka watu wote tumalize safari yetu ya duniani vizuri. Maana heri kuwa na mwisho mzuri kuliko kuwa na mwanzo mzuri kisha mwisho mbaya. Maisha ya toba yanatupatia mwisho mzuri (m.31, Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli?).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz